![]() |
| Naibu waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni vibaka na kumpora Wallet na kadi 6 za benki usiku wa kuamkia leo ikiwa ni saa chache tu zikiwa zimesalia kuanza kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kote nchini leo Jumapili Desemba 14,2014. Akizungumza na Malunde1 blog hivi punde Masele amesema tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 4 usiku wakati akishuka kwenye gari lake ili kuingia katika zahanati ya Majengo mjini Shinyanga kwa ajili yakupata matibabu kwani alikuwa anajisikia kuumwa baada ya kampeni za uchaguzi kumalizika. "Ghafla nilivamia na watu na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka,walinidhibiti katikati ya mlango wa zahanati na kunipora simu yangu ya mkononi yenye line ya Voda na Tigo,pochi yangu ya kuhifadhia pesa,lakini nawashukuru askari wa jeshi la polisi waliokuwa doria kwa kufika haraka eneo la tukio na kunipa msaada",aliiambia Malunde1 blog. "Naomba wananchi wawe watulivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi",aliongeza Mheshimiwa Masele. Hata hivyo kuna taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mheshimiwa Masele alifanyiwa vurugu wakati akitoa rushwa kwa wananchi Moja ya taarifa hizo ni hii hapa chini kutoka Jamii Forums Naibu waziri wa nishati akamatwa akigawa rushwa
Malunde1 blog imeongea na Masele hivi punde kujua kama taarifa hizo kuhusu kutoa rushwa zilizozagaa mtandaoni kama ni za kweli au la!!
"Ndugu yangu Malunde usihangaike na hao watu,wanataka kuleta mambo ya siasa tu,mimi sijafanya hivyo kama wanavyodai,kwanza hapo Dispensari, nilikuwa peke yangu,nilikuwa nimeenda kutafuta dawa/kupata matibabu baada ya kula chakula cha usiku kwani nilikuwa najisikia kuumwa ,nimeibiwa simu moja,kwenye pochi kulikuwa na kadi 6 za benki na pesa za Afrika Kusini Land 400 ambazo ni sawa na kama shilingi elfu 40 au 50 hivi ya Tanzania,wala sijaumia popote". Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Na Kadama Malunde-Shinyanga Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI |

Social Plugin