MOROGORO YAKUMBWA NA MAFURIKO LEO

Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka. 


Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.
Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika maji na kulazimika kuvutwa.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe  kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya wananchi.
via>> itv.co.tz

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527