PICHA 10 NA HABARI KAMILI KUHUSU MAHABUSU ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKITOROKA MAHAKAMANI JIJINI DAR ES SALAAM


kisutu 3
Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la ABDUL KOROMA Raia wa Siera Leone Ambaye alikuwa mahabusu katika gereza la keko jijini Dar es salaam ameuawa kwa kupigwa risasi na askari magereza katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu alikpokuwa akijaribu kutoroka.



Mahabusu huyo alikuwa anakabiliwa na tuhuma za Dawa za kulevya ambapo tukio hilo limetokea baada ya mahabusu kufunguliwa kutoka kwenye chumba cha mahabusu ya mahakama hiyo kuelekea kwenye gari la mahabusu ambapo Mara baada ya kutoka nje alianza kutimua mbio.
Kwa mujibu wa mashuhuda walio shuhudia tukio hilo wamedai kuwa wakati anaanza kukimbia askari magereza alifyatua risasi moja hewani bila mafanikio ndipo akampiga ya mkononi lakini bado akawa anakimbia na hivyo kutuka kwenye uzio kwa lengo la kukimbia Ng'ambo ya pili.

Mtu huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na kushitakiwa.

Ameuawa katika uzio wa Mahakama hiyo baada ya kumtoroka askari magereza aliyekuwa amemsindikiza kujisaidia ambapo alijaribu kuruka ukuta wa mahakama hiyo.

Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema; “alikimbilia kwenye ule ukuta pale, akapandisha mpaka pale juu… anataka arukie upande wa pili magereza washatokea, wakaona hawawezi kukimbia yuko mbali ndio wakampiga zile risasi kama tatu hivi ndio akafariki…

Akizungumzia tukio hilo Msimamizi wa Mashtaka Mahakama ya Kisutu Tumaini Kweka amesema; “Wakati wapo kwenye sero ndipo yeye akajaribu kutoroka kwa kujaribu kuruka ule ukuta wetu wa Mahakama ndipo wanausalama wetu ambao wako hapa wakaweza kundhibiti…

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleimani Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo chake
Muonekano wa mahabusu aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone baada ya kupigwa risasi.
Koroma akiwa  kwenye machela tayari kwa kupelekwa kuifadhiwa hospitalini.
Askari wakimuondoa mahabusu huyo.
Wananchi na Askari wakiwa eneo la tukio.
 Kisutu 4
Kisutu 5
Kisutu 1



kisutu 2
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527