ANGALIA PICHA_ HAIJAWAHI KUTOKEA,WASANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI BHUDAGALA MWANAMALONJA NA MCHELE MCHELE WAKUTANA LIVEE!! | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 15, 2014

ANGALIA PICHA_ HAIJAWAHI KUTOKEA,WASANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI BHUDAGALA MWANAMALONJA NA MCHELE MCHELE WAKUTANA LIVEE!!

  Unknown       Monday, December 15, 2014
Haijawahi kutokea Kanda ya Ziwa ndiyo maneno yaliyotawala leo katika eneo la Kisesa Mkoani Mwanza.Mapema leo wasanii maarufu/waimbaji wa nyimbo za asili hususani kabila la Kisukuma maarufu sana katika kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla leo wamekutana kila mmoja na kundi lake. Bhudagala Mwanamalonja na kikundi chake kutoka Serengeti mkoa wa Mara mapema leo asubuhi alimtembelea msanii mwenzake  Mchelemchele anayeishi Kisesa mkoani Mwanza.
Hapa zoezi la kutambulishana kundi la Bhudagala Mwanamalonja na kundi la Mchelemchele

Katikati ni Bhudagala Mwanamalonja,Kulia ni Mchele Mchele,kushoto ni DJ Jelly wakiwa katika picha ya pamoja.Wasanii hawa wanasifika kwa kutunga nyimbo zenye ujumbe mzito,lakini mbali na kuwa na uwezo wa kutunga nyimbo wasanii hawa wana uwezo mkubwa wa kucheza  na wamejaariwa kuwa na wanenguaji wazuri.Hakika kama umewahi kushuhudia Show zao ama kuangalia video zao utakuwa shahidi mzuri kwa hiki ninachokuambia
 
Wanaendelea kutambulishana
Aliyeshika upinde ni Mchelemchele,kulia kwake ni Bhudagala Mwanamalonja

Bhudagala Mwanamalonja hivi sasa anatamba na nyimbo mbalimbali kama vile Kundi wa Ng'wamoto,Kanisani unapiga simu,Bhujingi,Mujini Nalisama,Nyabhulugu,Mashaka,Izumo,Rusia,Gomis,Zaina,Mele,Mapolu,Bhabha Shokaga,Ng'wanamalonja,Mama Rhoda, Ng'wanambelele na Amani, huku Mchelechele naye akijizolea umaarufu kwa nyimbo zake nyingi kama vile Ng'wana wa Ntemi,Wanafunzi,Alinilelela,Lushikulumo,

Mchelemchele na Bhudagala Mwanamalonja watafanya Show ya kufunga na kufungua mwaka tarehe 25.12.2014 ,siku ya sikukuu ya Krismas huko Ngudu Mjini na  tarehe 01.01.2015 watafanya show Magu mjini kwenye uwanja wa mpira wa miguu

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post