ANGALIA PICHA_ MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHIRIKA LA AGAPE AIDS CONTROL PROGRAMME LEO MJINI SHINYANGA

 BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Hapa ni katika ukumbi wa Ibanza Hotel mjini Shinyanga ambako leo  kumefanyika mkutano mkuu wa mwaka wa Shirika la Agape Aids Control Programme(AACP),ambalo ni shirika lisilo la kiserikali,kisiasa wala kidini linalojihusisha na kuratibu masuala ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na madhara ya UKIMWI katika mkakakati wa haki za binadamu lenye makao yake mkabala na SIMEJ Hotel,mtaa wa Lubaga,kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga-picha na Kadama Malunde




Wafanyakazi wa shirika la AGAPE mkoa wa Shinyanga wakijitambulisha kwenye mkutano mkuu wa mwaka leo,aliyeshikilia kipaza sauti ni afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu-picha na Kadama Malunde
Aliyeshikilia kipaza sauti ni mwanasheria kutoka shirika la AGAPE Revocatus Robert akizugumza katika mkutano huo,ambapo miongoni mwa sababu zinasababisha kuendelea kuwepo ukatili kwa wanawake katika maeneo ya vijijini ni lugha ya Kiswahili kwani wengine wanashindwa kujitetea kutokana na hofu ya lugha hivyo shirika hilo linatoa msaada wa kisheria katika jamii-picha na Kadama Malunde
Imeelezwa pia kuwa changamoto kubwa katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia ni rushwa kutawala mahakamani,shuleni na kwenye familia matokeo yake wahanga wanapoteza haki zao za msingi-picha na Kadama Malunde
Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu akizungumza katika mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu,wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga-picha na Kadama Malunde
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini-picha na Kadama Malunde
Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu alisema mila na desturi potofu hususani kwa mtoto wa kike  bado ni kikwazo katika kuzuia ndoa na mimba za utotoni mfano Bukwilima,Samba n.k-picha na Kadama Malunde
Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu akizungumza katika mkutano huo ambapoalisema unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike kwa upande mwingine unasababishwa na ukosefu wa mabweni katika shule za sekondari  kitu ambacho huwalazimu kupanga ama kusafiri umbali mrefu kila siku matokeo yake wanafunzi wengi wa kike hujikuta wakijiingiza katika mahusiano ya mapenzi na watu wazima na kubebeshwa ujauzito-picha na Kadama Malunde
Mkutano unaendelea-picha na Kadama Malunde
Akina mama kutoka Chibe katika manispaa ya Shinyanga wakiimba nyimbo kuhusu ukatili wa kijinsia-picha na Kadama Malunde
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE mkoa wa Shinyanga John Myola akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema mkoa wa Shinyanga umekithiri kwa matukio ya watoto kuachishwa masomo na kupewa ujauzito na ndoa za utotoni.Alisema kila siku watoto 16 wanabakwa mkoani Shinyanga na wengine 500  kila mwaka wanapewa mimba na kuolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18-picha na Kadama Malunde

 BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527