Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA-AJALI YA BASI LA WIBONELA LEO ASUBUHI MJINI KAHAMA,WATU WANNE WAFARIKI DUNIA

Huzuni na majonzi imetanda asubuhi hii katika mji wa Kahama baada ya bus la Wibonela Express linalofanya safari zake  Kahama mkoani Shinyanga  kwenda Dar es salaam kupinduka baada ya kutoka Stand kuu ya Kahama  kilomita chache kutoka stand katika eneo la Phantom  na kuua watu wanne akiwemo mtoto mmoja,wanaume wawili na mwanamke mmoja na watu zaidi ya 40 kujeruhiwa.

Taarifa za awali zinasema chanzo cha  ajali hiyo ni mwendo kasi ,huku ikitajwa kuwa dereva alishindwa kulihili basi hilo na kupinduka katika kona ya Phantom
.
Uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kahama umesema waliofariki dunia ni watu wanne majeruhi 41.

>>BOFYA>>HABARI ZAIDI

ANGALIA PICHA ZAIDI HAPA CHINI





















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com