Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ACT tishio Shinyanga!! YAVUNA TENA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM,CUF NA CHADEMA

Kulia ni katibu mwenezi wa ACT mkoa wa Shinyanga Paul John Masanja akiwakabidhi kadi za ACT waliokuwa wanachama na viongozi wa CHADEMA,CUF na CCM katika ofisi za chama hicho-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog 

Waliokuwa CHADEMA,CCM na CUF  wakikadhiwa kadi za ACT baada ya kuhamia chama hicho-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog 
 Kulia ni katibu mwenezi wa ACT mkoa wa Shinyanga Paul John Masanja akipokea kadi za waliokuwa wanachama na viongozi wa CHADEMA,CUF na CCM katika ofisi za chama hicho-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog 
 Kulia ni katibu mwenezi wa ACT mkoa wa Shinyanga Paul John Masanja akiw ameshikilia kadi za waliokuwa wanachama na viongozi wa CHADEMA,CUF na CCM-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog 

Chama kipya cha Aliance for Change and Transarency (ACT),Tanzania Mjini Shinyanga mkoani Shinyanga, kimesajiri wanachama wapya wa vyama vya upinzani, Cuf, Chadema,CCM, pamoja na kuwa kabidhi kadi  kuwa wanachama halali wa Chama hicho.
 
Wanachama hao walikabidhiwa kadi za ACT juzi mbele ya waandishi wa habari mjini Shinyanga.
 
Waliotimkia ACT ni , wanachama hao wapya waliotoka CCM, ambao ni Samweli Chanuo, Neema Benard, Samaka Andrew, Juma Moshi, Juma Yegela,Edward Alex(wote kutoka CCM) na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM, tawi la kitangiri Mjini Shinyanga.
 
Wanachama wengine waliohama vyama vyao na kujiunga na ACT ni Rose Mary, aliyekuwa mwanachama wa Cuf, pamoja na Magdalena Benard , aliyekuwa katibu wa baraza la wanawake Chadema (BAWACHA), kutoka kata ya Ndala mjini Shinyanga.
 
Hata hivyo waliokuwa wanachama wa CCM, wameelezea sababu za kukihama chama hicho na kujiunga ACT, ambapo walitoa sababu mbalimbali kwa nyakati tofauti, lakini moja ya sababu kuu, walisema CCM, imekuwa na sera mbovu, na kutotekeleza ahadi zake kwa wananchi , kama inavyoahidi inapokuwa ina nadi sera zake.
 
Nao waliokuwa wanachama wa Chadema na Cuf,  walisema  vyama hivyo ,vimekuwa havina mwelekeo wa kuleta ukombozi kwa wananchi na matokeo yake vimekuwa na tabia ya kuchafuana ndani ya chama, kutokana na kugombania nyadhifa za uongozi, hali ambayo imekuwa ikisababisha   mgongano wa kimaslahi na kuleta vurugu ndani yake.
 
“Sisi kwa hiari yetu bila ya kushinikizwa na mtu yeyote tumeamua, kujiunga na chama kipya cha ACT, na kuwa wanachama wapya, chama ambacho tumevutiwa na sera yake ya ukweli na uwazi, hivyo tuna amini chama hiki ndio mkombozi wa watanzania” walisema kwa nyakati tofauti wanachama hao wapya wa ACT.
 
Katibu wa wilaya ya shinyanga Mjini Charles Sangura, alisema hana taarifa juu ya wanachama wake kuhamia ACT, na hayupo tayari kulizungumzia suala hilo.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini Hassani Baruti, amekiri kumtambua Magdalena Benard,aliyekuwa katibu wa baraza la wanawake Chadema (BAWACHA), kutoka kata ya Ndala mjini Shinyanga aliyehamia ACT.
 
Hata hivyo Baruti alisema kuwa mtu huyo, tangu awali alikuwa siyo mwanachama mzuri , na alikuwa katika hatua za mwisho , hivyo ameamua kujisalimisha mapema kabla ya chama kumchukulia hatua.
 
Naye katibu mwenezi wa Chama cha ACT, mkoani Shinyanga, John Paul Masanja na mwenyekiti mpya wa chama hicho wilaya Godwin Makomba, wamethibitisha kuwapokea wanachama hao, pamoja na kuwapa kadi na kuwa wanachama halali wa ACT, na kusema kuwa chama hicho kinaendelea kukua kila kukicha na wananchi wategemee ukombozi wa maendeleo.

Habari na  Kadama Malunde-Shinyanga


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com