Jengo la wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga Complex)
Moto mkubwa uliozuka leo mchana katika jengo la biashara Machinga Complex Ilala jijini Dar es salaam, umedhibitiwa baada ya kutekeza mali katika baadhi ya maduka.
Mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa jengo la Machinga Complex, Godwin Mmbaya amesema moto huo umedhibitiwa na hali ni shwari.
“Tunashukuru Mungu moto umedhibitiwa kabla haujasambaa zaidi, kikosi cha zimamoto kiliwahi mapema na kilisaidia kufanikisha kuzima moto. Hakuna mtu alieyeumia zaidi ya kuteketea kwa mali kwenye maduka ambayo moto ulitokea, bado hatuna tathimini ya mali zilizoteketea, chanzo cha moto ni fundi alikuwa anakata kitu na mashine sasa vile cheche zikadondokea kwenye kitu, moto ukatokea na kuchanganya, sisi kwanza tunawapa pole wale wote waliopotelewa na mali zao kwa moto,” alisema Godwin.
Katika hatua nyingine Godwin alisema material yaliyotumika kujengea jengo hilo ni material ambayo hayawezi ungua na moto hali iliyosaidia moto huo kutosambaa mbali zaidi

Social Plugin