TAARIFA KAMILI KUHUSU SAKATA LA NESI KUDAIWA KUCHANGIA KUUA WATOTO MAPACHA WODINI,HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA
Friday, September 26, 2014
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Dkt Ntuli Kapologwe kuhusu sakata la nesi kudaiwa kuchangia vifo vya watoto wawili mapacha kutokana na kile kichodaiwa kuwa nesi alikuwa bize na simu.Dkt Mlekwa amesema wamebaini kuwa mimba ilikuwa na miezi 6 na ilikuwa imeharibika na kwamba,mama anayedaiwa kujifungua ana miaka 15,mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Mwasele.Dkt Mlekwa ameongeza kuwa watoto waliozaliwa mmoja alikuwa na uzito wa gramu 500,wa pili gramu 700 ambapo kimsingi hawawezi kuishi na kwamba nesi aliyetupiwa lawama alikuwa ameshawapa taarifa ndugu wa binti kuwa mimba imeharibika lakini hawakutaka kuelewa.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Binti aliyejifungua watoto mapacha,ambaye amekiri kujifungua watoto wadogo sana tofauti na watoto wengine wanaozaliwa.Amesema alijifungua mtoto wa kwanza mdogo sana akiwa amekufa na wa pili akiwa hai lakini alifariki baadaye.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin