JAMII YATAKIWA KUACHA KUFUMBIA MACHO VITENDO VIOVU DHIDI YA WATOTO



Jamii wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuwa na uelewa juu vitendo viovu wanavyotendewa watoto wa kike na baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na kutovifumbia macho ili kuisaidia Serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa Wilaya hiyo,Benson Mpesya wakati akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa kutokana na kukithili kwa mimba za utotoni huku wakiwa mashuleni.

Aidha Mpesya amewataka wazazi kuepuke kupokea vitu vidogovidogo pamoja na kuwaoza watoto wao wakiwa katika umri mdogo huku wakiwa bado wanasoma ni kukiuka sheria ambapo ameahidi kuyatafuta majalada ya kesi hiyo na kuesma endapo iliendeshwa kinyume utaratibu itarudiwa.



Hivyo ameitaka jamii kwa kushirikiana na Serikali kufanya kazi na shirika hilo ili kuibua maovu yanayoendelea kwenye jamii hiyo ili kuleta mabadiliko katika usawa wa kijinsia.


Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka shirika la CARE INTERNATIONAL,Gega Bujeje amesema shirika lake linajihusisha katika kutoa elimu ya Afya na uzazi pamoja kupinga mimba na ndoa za utotoni na amedai kuwa wanakumbana na changamoto nyingi katika jamii kutokana na uelewa mdogo wa wazazi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post