MREMBO ABAKWA BAADA YA KUPEWA LIFTI KWENYE GARI

Mwanamke mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 22 mkaazi wa Mjini Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba amebakwa na kisha kutelekezwa na dereva wa gari lilikokuwa limempa msaada wa lifti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amesema tayari jeshi hilo linamshikilia Mohammed Kaithar Ali (45) Mkaazi wa Wete ambaye anatuhumiwa kuhusika na kitendo hicho. 

Imedaiwa kuwa Mohammed ametenda unyama huo jana majira ya saa kumi jioni katika eneo la Weni Wete. 

Shekhan amesema mtuhumiwa ametekeleza kitendo hicho baada ya kuombwa lifti na alipofika maeneo ya Weni kijana huyo alifunga vioo vya gari lake na kisha kumziba mdomo ili sauti isitoke. 

Kamanda Shekhan amesema msichana huyo amepata maumivu sehemu zake za siri pamoja na kupata michubuko shingoni, ambayo imetokana na harakati za kutaka kujinasua ili asifanyiwe kitendo hicho.

via>>Farajimfinaga.com

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post