MFANYABIASHARA AMCHARANGA MAPANGA ALBINO MSITUNI HUKO MOROGORO

Mlemavu wa ngozi Damas Valeniani aliyecharangwa mapanga na mfanyabiashara maarufu mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina moja la Lyimo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro likimshikilia mkazi wa wilayani Mvomero, Johnson Damian Mkude kwa msala wa kumchinja mdogo wake na kupeleka kichwa kwa mganga wa kienyeji ili awe bilionea, jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara mwingine maarufu mkoani humo aitwaye Lyimo kwa tuhuma za kumcharanga mapanga Damas Valeniani (36) ambaye ni  mlemavu wa ngozi (albino). 

Jamaa huyo maarufu kwa jina la Mangi, anadaiwa kutenda unyama huo wiki iliyopita usiku wa manane kwenye Msitu wa Milima ya Uluguru, Mtaa wa Bingwa Kiwasi Juu, Kilakala, wakati mlemavu huyo, akiwa amelala. 


“Nilikuwa nimelala, ghafla nikasikia mtu akiingia akiwa ameshika panga na kuanza kunikatakata huku akitaka kuninyofoa masikio yangu. 

Nilimtambua kuwa ni Lyimo ambaye ni jirani yetu.

SOMA HABARI HII HAPA

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post