MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI YAANZA KUWASHUGHULIKIA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII

TCRA yaanza kuwashughulikia wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii
Mamlaka  ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuwakumbusha wananchi  kutumia njia ya mawasiliano ipasavyo ili kujijengea heshima kwani kwa sasa hatua kali za kisheria zimeanza kuchukuliwa kwa wale wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Times fm,  Meneja mawasiliano wa  (TCRA) Inocent Mungy amesema kuwa ipo haja kwa wasichana kujiheshimu kwani picha nyingi mbaya zinazoonekana kwenye mitandao hiyo  ni zao.
Naye Mkuu wa kitengo cha masuala ya watumiaji wa mitandao Isack Mruma amesema watu wanapaswa kuelewa matumizi  sahihi ya mitandao na lazima kuwe na usiri wa akaunti za mitandao ili kuweza kuepukana na matatizo ya usambazaji wa picha mbaya kwenye mitandao hiyo.

UNGANA NASI KWA KU LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA MOJA,BONYEZA MANENO HAYA SASA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527