Maandamano yaliyotangazwa na Chadema mkoa wa Shinyanga yaliyopangwa kufanyika leo saa mbili asubuhi,yameishia pasipojulikana baada ya viongozi wa Chama hicho kufunga ofisi yao na kutojulikana walipokuwa na baada ya kutafutwa na waandishi wa habari kujua kulikoni hawaonekani wakati wametangaza kuandamana,mwenyekiti wa chama hicho mkoa Peter Machanga alidai kuwa leo walikuwa wanawaandaa tu wananchi kwa ajili ya maandamano yatakayotangazwa rasmi. Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Shinyanga mjini walisema huenda maandamano hayo yamesitishwa kutokana na askari wa jeshi la polisi kutapakaa mitaani kwa ajili ya kukabiliana na yeyote mwenye kujitokeza kuandamana. Pichani ni ofisi ya Chadema ikiwa imefungwa leo BONYEZA HAPA KUONA HALI ILIVYOKUWA LEO MJINI SHINYANGA |