MENEJA WA MAN UNITED ATOA SABABU YA KUFUNGWA GOLI 5


Meneja wa Man Utd, Aloysius Paulus Maria van Gaal amesema ameshangazwa na hatua ya wachezaji wake kuridhika na mabao matatu ambayo walikuwa wakiongoza, na mwishowe walimaini mambo yamekwisha. 


Louis van Gaal amesema kutokana na kitendo hicho kikosi chake kilistahili kuadhibiwa kutokana na wapinzani kuonyesha kujituma wakati wote na mwisho wa dakika 90 lengo lao lilitimia kwa kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao matano. 

Amesema aliamini walivyoanza vyema katika mchezo uliopita dhidi ya QPR kutokana na kuwa na wachezaji aliowasajili mambo yangeendelea kwa nidhamu ya mchezo kama walivyocheza Old Trffortd, lakini matokeo yake wameambualia aibu na sasa hana budi kujipanga upya kwa ajili ya mchezo ujao ambapo watapambana na wagonga nyundo kutoka magharibi mwa jijini London West Ham Utd.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post