WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WABURUZWA MAHAKAMANI

Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya ya Geita katika idara  ya misitu wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Geita baada ya kupatikana na tuhuma 30 likiwemo la kusababishia hasara kwa mwajiri wake kiasi cha shilingi milioni 229,866,400/=

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya Desidery Kamugisha ,mwendesha mashtaka wa serikali Enosi Erasto alisema kuwa mnamo mwez wa sita mwaka 2009 na mwezi wa 12 mwaka 2011 huko katika msitu wa akiba wa Geita  kwa mida tofauti tofauti  washitakiwa hao wakijua ni kosa la jinai na kwa maksudi   walitenda makosa hayo na kusababisha hasara kubwa kwa mwajiri wao.

Mwendesha mashitaka huyo ameongeza kuwa mara baada ya kutenda makosa hayo kwa makusudi pamoja na kutenda makosa hayo hawakuweza kutoa taarifa yoyote ya ukweli kwa mwajiri wao na hivyo wakamdanganya.

Aidha watuhumiwa hao ambao ni  Emanueli Mabala,Kasika Gamba,Elizakayo Yobu shuma, Alexanda Makali Masawe, Paulo Maganya, wote wakiwa ni watumishi  hiyo katika wilaya ya Geita.

Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo kwa mara ya kwanza kwa hakimu Kamugisha  washitakiwa hawakujibu chochote kutokana na ushahidi kutokmilika na walipelekwa rumande mara baada ya kukosa vigezo vya dhamana na kesi yao itasikilizwa tena tarehe 07 mwezi wa nane mwaka huu.

Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527