TAZAMA PICHA_MAKINDO HOTEL YA SHINYANGA YAMVUTIA MSANII JOHARI WA BONGO MOVIES

Pichani ni mkongwe wa maigizo na filamu za Kibongo, Blandina Chagula (Johari) amezaliwa mkoani Shinyanga ambaye katika safari yake ya kuelekea wilayani Maswa mkoa mpya wa Simiyu ameamua kufika  “MAKINDO COMMERCIAL HOTEL” na kulala Hotel hiyo ya Kisasa.Johari ameeleza kufurahishwa na huduma nzuri katika hoteli hiyo na kuongeza kuwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wana kila sababu ya kujipongeza kwa maendeleo waliyofikia kwa kuwa na Hotel ya kisasa ukilinganisha na siku za nyuma ambapo mkoa ulionekana kuwa nyuma kimaendeleo.

"Kwa kweli hoteli hii ni nzuri,Shinyanga tunapiga hatua,sasa tuna hotel ya kisasa,tena imejengwa na wazawa wa Shinyanga",alisema Johari
Hapa ni ndani ya moja ya vyumba katika Hoteli ya Makindo “MAKINDO COMMERCIAL HOTEL” iliyopo katika eneo la Majengo mjini Shinyanga.Ipo nyuma ya Vijana Senta karibu na Bakurutu mjini Shinyanga.Ni hotel ya kisasa ambayo imepata umaarufu mkubwa siku chache tu baada ya kuzinduliwa mwezi Juni mwaka huu 2014.Hotel hii ya kisasa imekuwa kivutio kikubwa kwa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa,dini,wafanyabiashara na watu mbalimbali wakiwemo wasanii kwani wahudumu wake ni wakarimu sana,huduma nzuri na bei zake ni za kawaida tu  ambapo vyumba vinapatikana kwa shilingi 30,000/=  na 25,000/=
Dressing Table ndani ya chumba-kama unavyoona pichani ni baadhi ya vitu utakavyovikuta katika vyumba,vingine ni pamoja na Tv flat screen,Air Condition,simu ,friji na kabati,lakini pia maji ya moto yapo. Hakika ukifika Makindo Commercial Hotel  utatamani kufika tena na tena kwani ni Hotel ya kisasa zaidi

Katikati ni msanii mkongwe kutoka Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ (aliyesoma shule ya msingi Bugoyi iliyopo mjini Shinyanga) akiwa katika picha ya kumbukumbu na mkurugenzi wa Makindo Commercial Hotel bwana Nehemia Makindo(kulia) kutoka Shinyanga leo katika hotel hiyo.Kushoto ni mmoja wa wahudumu katika hotel hiyo bi Mariam Mathew
Popote pale ulipo unaweza kuwasiliana na wahusika wa Makindo Commercial Hotel ya mjini Shinyanga kwa kupiga simu namba 0767 165 475 au 0787 165 477 au 0753 178 221



Nje ya Makindo Commercial Hotel ambapo kuna nafasi pia kwa ajili ya kupaki vyombo vya usafiri


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post