MASKINI_ MGANGA WA KIENYEJI ATOWEKA NA SEHEMU ZA SIRI ZA MTOTO HUYU

Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Katika hali ya kushangaza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam walipigwa na butwaa baada ya mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa seheme zake za siri na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji na kukimbilia kusikojulikana.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Alisema mganga huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.

“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia mwanangu.

Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.

“Pia nilikwenda Kituo cha Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba huyo
Mzazi huyo aliiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande wake, muuguzi wa zamu aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Kwa ujumla huyu mtoto amebadilishiwa staili ya maisha na hicho ni kilema. Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika maisha yake,” alisema muuguzi huyo.

Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527