MWANAFUNZI WA MLIMANI (UDSM) AFARIKI DUNIA GHAFLA ,TAZAMA PICHA HAPA



Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam  aliyejulikana kwa jina la Sakabenga (pichani enzi za uhai wake) amefariki dunia jioni hii akiwa amelala bwenini chuoni.


Mwanafunzi huyo wa Kike wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam amekutwa amefariki akiwa amelala kitandani chumba cha hostel, Inasemekana aliwaaga wenzake kuwa anakwenda kupumzika kidogo baada ya vipindi, baada ya muda wenzake walimkuta kitandani akiwa kishafariki



Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Sakabenga amefariki akiwa amepumzika chumbani kwake na sababu za kifo hicho hazijajulikana

Mwili huo wa marehemu tayari umechukuliwa na umepakiwa kwenye gari tayari kwenda kuhifadhiwa


Taarifa kamili iko hapa chini

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Happiness Sakabenga, jana amefariki ghafla chumbani kwake baada ya kutoka kwenye vipindi vya masomo asubuhi, chuoni hapo.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili aliyekuwa akichukua Shahada ya kwanza ya Biashara na Uhasibu, baada ya kutoka darasani alikwenda kupumzika na hakuamka tena.

Habari za ndani kutoka kwa marafiki zake zinasema  kuwa mwanafunzi huyo alitoka darasani majira ya saa 5 asubuhi na kuwaomba wenzake wamuamshe saa 6 mchana baada ya kupumzika.

Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa wanafunzi wenzake walipokwenda kumwamsha, alikuwa amekwisha fariki dunia.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema Happiness alihudhuria vipindi vya asubuhi na baada ya kutoka darasani aliwaambia wenzake kuwa anakwenda kupumzika.

Rais wa serikali ya wanafunzi UDSM, Filbert Nickson, alisema mwanafunzi huyo asubuhi alikuwa mzima akiendelea na shughuli zake mpaka alipokutwa amefariki dunia.

Nickson alisema wanafunzi walitoa taarifa kwa madaktari wa chuo na ndipo mwili huo ulipochukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema madaktari wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi mwili huo  na taarifa ya sababu ya kifo hicho itatolewa. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Thobias Tedoyeka, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema maafisa wa polisi wapo chuoni hapo kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527