Utafiti!! VIPIMO VYA DNA VYAONESHA WANAUME WENGI WANACHEPUKA KATIKA MAHUSIANO YAO

Hii inaweza kuleta ugomvi wa fikra kati ya uhalisia na utafiti wa wanasayansi katika dunia hii inayoendeshwa na mambo mengi yaliyogunduliwa na wanasayansi, lakini…amini usiamini hiki ndicho kilichoonekana kwenye vipimo vyao.
Wanasayansi wa chuo cha West Manchester cha Uingereza ambao wamebobea kwenye masuala ya saikolojia na biology, wametumia kipimo cha vinasaba ‘DNA’ kufanya utafiti uliohusisha saikolojia na biology ya binadamu na kugundua kuwa karibu wanaume wote wanachepuka katika mahusiano yao.
 Wanasayansi hao wamekuwa wakifanya utafiki wa vinasaba kwa makundi mbalimbali ya wanaume kwa lengo la kufahamu utofauti wa kisaikolojia kati ya wanaume na wanawake katika mahusiano.
Kwa mujibu wa utafiti huo ulioripotiwa na mtandao MapeNation uliopata copy iliyokusudiwa kupelekwa kwenye vyombo vya habari, wanasayansi hao walitumia vipimo vya vinasaba vinavyopatikana katika meno makali ya mbele ya mbwa ‘canine teeth’ ambayo yameelezwa kutumika katika kuzalisha madini ya proteins na nucleic acids, ambazo huongeza hali ya mbwa kutaka kuwa na mwenza wake kwa kiwango cha juu.
Baada ya majaribio kadhaa, walihitimisha kuwa takribani miaka 200,000 iliyopita aina ya mbwa aina wenye meno makali walikuwa wakiwinda wanyama kwa ajili ya chakula. Kadri muda ulivyozidi kwenda wanyama hao walitengeneza vinasaba ambavyo vinaendana na vile vya wanyama hao waliokuwa wakiwawinda na kuwala, na vina hivyo vilitumika kama kinga dhidi ya wanyama wenzao wanaowala (predators).
Imeeleza kuwa wanyama hao waliotengeneza vinasaba hivyo walivyozidi kusambaa na kujikuta wakiliwa na binadamu wa sasa. Na mwisho binadamu hao wameendelea kubeba vinasaba vinavyobeba virutubisho vilivyozalishwa na wanyama hao (biopolymer).
Matokeo yake, binadamu (wanaume) walirithi vitu vinavyosababisha msukumo/khari ya kutaka kuwa na wenza hali inayowapelekea kusaka wanawake kadri iwezekanavyo wakati huo.
Mwandishi wa mtandao wa MapeNation aliyejitambulisha kwa jina la Zay alimuomba Dr. Yus I. Birchmier atoe ufafanuzi rahisi kuhusu utafiti huo na akaeza kuwa inaonesha kuwa tabia ya kuchepuka aka kusaliti kaika uhusiano wa mapenzi iko kwenye vinasaba vya mwanaume.
“Well, essentially, it means that it is in a man’s DNA to cheat.  It can no longer be denied.  The DNA links prove it.” Alieleza Dr. Yus.
Hata hivyo, walipoulizwa wanaume kadhaa kuhusu majibu hayo wengi walionekana kuchukizwa nayo huku baadhi wakiyafurahia.
 “It’s bullsh-t! It’s just another thing for females to throw in our face! They should have kept this sh-t secret!” alisema Clyde Williams.
Matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutangazwa rasmi wiki kadhaa zijazo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post