TUKIO LA MAHAFALI YA CHUO CHA UALIMU SHINYANGA,MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAHUDHURIA NA KUTOA ZAWADI KWA WAHITIMU


Ni katika viwanja vya Chuo cha ualimu cha Shycom mjini Shinyanga ambako jana kumefanyika mahafali ya sita ya chuo hicho kikongwe chenye wanafunzi zaidi ya 500  kilichoanzishwa 1965,Mbele upande wa kushoto ni katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo bwana Projectus Lubanzigwa katika kati ni mkuu wa chuo cha Shy-com bwana Paschal  Highmagway akifuatiwa na meneja wa kumbukumbu kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund),bwana Chacha Nyaikwabe wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mahafali hayo,ambapo pamoja na mambo mengine PSPF ilitoa zawadi kwa wahitimu.
Wahitimu 125  wa chuo cha ualimu cha Shinyanga(Shy-com) ngazi ya cheti na diploma wakiwa katika eneo la mahafali ambao katika risala yao walisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uzio na miundombinu mibovu ya jiko hali inayosababisha wakati mwingine kula chakula kibichi
Aliyesimama ni mkuu wa chuo cha ualimu cha Shinyanga(Shy-com) bwana Paschal  Highmagway akisoma taarifa ya chuo hicho kilichoanzishwa  1965 na mpaka sasa kina jumla ya wanafunzi 566 na wakufunzi 32 wakike 10 wa kiume 22

Meneja wa kumbukumbu kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund),bwana Chacha Nyaikwabe akizungumza katika mahafali hayo ambapo alisema kutokana na mfuko wa pensheni wa PSPF kutambua kuwa walimu ndiyo wadau wakubwa wa mfuko huo mfano hivi sasa aslimia 97 ya walimu wote nchini ni wananchama wake ,na kati ya wanachama wote wa mfuko walimu ni asilimia 67 hivyo wameona umuhimu wa kuwafikia na kuwapatia zawadi ili kuonesha kuwa inawatambua na kuwajali.
 Alizitaja zawadi  walizozitoa kwa wanafunzi waliohitimu chuo cha Shycom kuwa hizo  ni shilingi laki tatu,cheti na t-shirt ya PSPF kwa mwanafunzi wa (kwanza) aliyefanya vizuri katika masomo yake,shilingi laki mbili,cheti na t-shirt ya PSPF kwa mwanafunzi wa pili,shilingi laki moja, ,cheti na t-shirt ya PSPF kwa mwanafunzi wa tatu.
Meneja wa kumbukumbu kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF makao makuu Dar es Salaam Chacha  Nyaikwabe akikabidhi zawadi ya  shilingi laki tatu,cheti na t-shirt ya PSPF kwa mwanafunzi  wa kwanza Amina aliyefanya vizuri zaidi katika masomo yake akipokea zawadi

Kulia ni bi Amina mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika masomo yake katika chuo cha Shycom mwaka huu akiwa ameshikilia zawadi zake kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF 
Meneja wa kumbukumbu kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF makao makuu Dar es Salaam Chacha  Nyaikwabe akishikana mkono na baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho waliofanya vizuri katika kuwafundisha wanafunzi hao.

Kushoto ni Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akishikana mkono na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Ualimu cha Shycom aliyemaliza muda wake baada ya kumaliza muda wake.Mbali na PSPF kutoa zawadi kwa wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika masomo yao pia ilitoa zawadi kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi ambapo rais aliyemaliza muda wake alipewa zawadi ya shilingi elfu hamsini na t-shirt ya PSPF na rais aliyepo alipatiwa T-shirt pamoja na shilingi laki moja kwa ajili ya stationaries.

Akizungumza katika mahafali hayo afisa huyo alitumia fursa hiyo ku
washauri wahitimu hao pale watakapoingia katika ajira wasilazimishwe kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka kwa waajiri wao bali wana haki ya kuchagua kujiunga na mifuko yoyote ile ambayo itawaboreshea maisha yao ya baadae hasa pale wanapostaafu na kwamba PSPF ndiyo chaguo sahihi.

picha zote na Marco Maduhu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post