MZEE MAJUTO NA HEMEDY PHD WASHUTI FILAMU YAO MPYA YA COMEDY INAITWA- "KIMBULU"

Hemedy amesema wameamua kushuti filamu hiyo jijini Mwanza ili kubadili mazingira na kuleta muonekano tofauti na ule wa Dar unaoonekana kwenye filamu nyingi.
“Watu wengi wamekuwa wakisema wamechoka kila siku kuona majengo ya Dar es Salaam, kwa hiyo tumeamua kubadilika kuja huku halafu Mwanza yenyewe sio town ni kidogo nje ya mji.

 Nafikiri kutokana na mandhari ya Mwanza mawe mawe mtu atakuwa anajua kabisa kwamba project imefanyika ndani ya Rock City.” Amesema Hemedy.
Ameelezea kuwa filamu hiyo inahusu vijana wawili ambao walikuwa wameenda kijijini kwa lengo la kutafuta vijana wanaojua kuigiza ili wawaunganishe na wasanii wakubwa wa mjini lakini mwisho wa siku vijana hao wageuka na kuendekeza uzinzi na kuwa wezi.
Vijana hao waliishia kwenye mikono ya wanakijiji waliowashambulia kwa kipigo kikali baada ya kukamatwa wakiiba kuku.
Amesema lengo la kuigiza filamu hiyo ni kufikisha ujumbe kwa wasanii wenzao kuwa kama wanaamua kusaidia watu wafanye hivyo na si vinginevyo.
“Kwa hiyo ni kuwafungua macho wale wote wanaotumika kwa style hiyo, na vilevile kuonesha wasanii kwamba kama tunaamua kusaidia tusaidie kweli na isiwe na isiwe watu tunawafanyia michezo mibaya kama hiyo.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post