MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA PAROKO WA GEITA ALIYEFARIKI GHAFLA

 Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Ibrahim Malwa akitoa heshima za mwaisho kwa marehemu

Mhashamu askofu Damian Dallu wa jimbo la Geita leo ameongoza ibada ya misa ya kumuombea na kumuaga marehemu padri Henry Kimisha aliyekuwa paroko wa parokia ya kanisa la mama fatima lililopo mjini Geita aliyefariki dunia ghafla mwezi huu kwa shinikizo la damu.

Akiongoza ibada hiyo leo iliyofanyika katika kanisa kuu jimbo la Geita Damiani Dallu  ambayo pia imehudhuriwa na askofu Marco Msonganzila kutoka jimbo la Musoma na askofu Renatus Nkwande wa jimbo la Bunda askofu Dallu amesema amewataka waumini kuiga mambo yote mazuri aliyoyafanya  Padri Kimisha katika uhai wake huku akiwataka kujiandaa wakati wote kwani haijulikani siku wala saa ya kufa.

Mhashamu askofu Damian Dallu amesema ni vyema wakristo wote wakajiandaa kwa kuwasaidia wahitaji na wajane na wenye shida mbalimba wangali wako hai akatoa mfano kuwa Kimisha aliwasaidia watu wengi wahitaji na wenye shida mbalimbali hivyo kuwataka wakristo kuiga mfano wake.
Amesema Padri Kimisha atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoyafanya katika parokia ya Geita kubwa ikiwa ni kuwahimiza vijana na wazee kufunga ndoa kuliko kukaa katika maisha ya kishetani.

Padiri Kimisha alizaliwa tarehe 8. 6. 1967 katika kijiji cha Katunguru wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza na alipata daraja la upadri  tarehe 25 .7. 1996 katika parokia ya Nyantakubwa Sengerema mkoa wa Mwanza na alifariki siku ya jumatatu  kwa shinikizo la damu katika hositari ya wilaya Geita na amezikwa leo kati makaburi ya kanisa la mama wa Fatima yalioko katika kanisa hilo.
 
Mazishi ya padri Kishisha yamehudhuriwa pia na viongozi wa serikali wakiwemo  naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dk,Charles Tizeba mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk,Evarist Ndikilo na mkuu wa  wilaya ya Geita Omari Mangochie,mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Ibrahimu Marwa na mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu pamoja na  mapadri,masisita,
waumini na watu wenye mapenzi mema kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita na mikoa jirani.


Mungu ailaze mahala pema mbinguni roho ya marehemu padri Kishisha.Amina!! 
 Na Valence Robert-Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post