HII HAPA NDIYO HOSPITALI YA WILAYA YA KISHAPU MKOANI SHINYANGA,MGEJA AITEMBELEA

Moja ya majengo katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga iliyopo katika eneo la Mhunze,inayotarajiwa kuanza kutumika mwezi Julai mwaka huu
Ni katika ziara yya a siku moja  mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja( wa pili kutoka kulia),jana wilayani kishapu mkoani Shinyanga,akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa siasa ya mkoa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ,hapo anasomea taarifa kuhusu ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kishapu muda mchache baada ya kuwasili eneo hilo kutembelea mradi huo na kuona umefikia hatua gani

Kulia ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,mbele ni katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Shinyanga ndugu Emmanuel Mlimandago,katikati ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nhambaku wakiangalia jinsi ujenzi wa hospitali ya wilaya unavyoendelea
Hili ni jengo jingine katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga

Hii ni sehemu ya kuoshea maiti katika jengo la mochwari katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.


Msafara wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati wa ziara yake wilayani Kishapu ukitoka kuangalia Jengo la mochwari ambako ndugu zetu walitangulia mbele za haki watakuwa wanaoshwa.

Jengo jingine likiendelea kujengwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akishiriki ujenzi  wa moja ya wodi ya wazazi katika jengo la hospitali ya wilaya ya Kishapu inayotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu.

Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga akishiriki ujenzi wa jengo kwa ajili ya wazazi alipokuwa kwenye ziara yake ya siku moja wilayani Kishapu kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2010.Akiwa katika ziara yake wilayani Kishapu Mgeja alikuwa ameambatana na viongozi wa kamati ya siasa mkoani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post