WANAFUNZI 1302 SHULE YA MSINGI KIDINDA MKOANI SIMIYU WANAKAA CHINI,DARASA MOJA KUKALIWA NA WANAFUNZI ZAIDI YA 200

 
Sekta ya elimu hapa nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi,ambapo  huko mkoani Simiyu wanafunzi 1302  katika shule ya msingi Kidinda iliyopo kata ya Bariadi katika halmashauri ya Mji wa Bariadi wanakaa chini kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa madawati kwa muda mrefu.

Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1622, wavulana wakiwa 807 na wasichana 815, mbali na kukabiliwa na upungufu huo wa madawati, bado madarasa ni machache hali inayosababisha zaidi ya wanafunzi 200 kujazana ndani ya chumba kimoja cha darasa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Josephina Sitta amesema kutokana na changamoto hizo shule yake ina jumla ya madawati 190 na  kila dawati  linakaliwa na wanafunzi 3, ambapo wanafunzi 570 ndiyo wanaokaa kwenye madawati, na wanafunzi 1302 wakiwa wanakaa chini hali inayosababisha kuwepo kwa upungufu wa madati 434.

Amesema kutokana na  kuongezeka  kwa wanafunzi kila mwaka  katika shule yake imesababisha shule hiyo inahitaji jumla ya vyumba vya madarsa 6, na sasa vyumba vya madarsa viko 11 hali inayopelekea darasa moja kutumiwa na wanafunzi zaidi ya 200.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post