Ukanjanja noumaa!!! TAZAMA PICHA ZA MWANDISHI FEKI ALIYENASWA AKITAKA KUTAPELI HUKO DODOMA

Mwandishi wa habari feki aliyejitambulisha kwa jina la Meshaki amejikuta kwenye wakati mgumu siku ya leo baada ya zoezi lake la kutaka kumtapeli mheshimiwa Shabiby na kujifanya yeye ni mhariri wa gazeti la dira ya mtanzania,
Mwandishi wa habari feki  akiwa mikononi mwa vyombo vya dola baada ya kushtukiwa:


Mhariri huyu feki alitumia janja ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno mh na kujitambulisha kuwa yeye ni mhariri mkuu wa gazeti la Dira

lakini zoezi hilo lilikuwa ngumu kufanikiwa kwa mhariri huyo feki baada ya mheshimiwa kumshtukia na pia alikuwa anamfahamu vizuri mhariri mkuu wa gazeti hilo, Mhariri feki huyo baada ya kuona ameshtukiwa aliamua kukiri na kuomba msamaha na kudai kuwa ni ugumu wa maisha ndio umemsababishia hali hiyo, 

Kutokana hali na huruma ya mheshimiwa shabiby aliyokuwa nayo aliamua kumsamehe na kumpatia fedha zaidi ya laki moja, Ila mhariri feki huyo anashikiwa na jeshi la polisi kwa kuadhalilisha taaluma hiyo na pia kulichafua gazeti hilo la Dira, Pia Mh Shabiby aliendelea kututonya kwamba kuna waandishi wengi ambao wanatumia janja hiyo ili kujipatia fedha na pia alituambia kwamba alishawahi kumshtukia mwandishi wa gazeti la Nipashe na baada ya kuona ameshtukiwa anaambiwa alitoka ndiki mithili ya swala na kuacha vumbi endeo hilo
Jeshi la polisi likifanya kazi yake

Mhariri feki akiwa kajificha kwa kuziba kichwa ili asipigwe picha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post