SITTA ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI BUNGE LA KATIBA KWA KISHINDO

 
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 469 dhidi ya mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita.
 
Katika kura hizo Mh. Hashim Rungwe ameambulia kura 69 pekee, huku Mh Samia Suluhu Hassan akipata nafasi ya Makamu mwenyekiti wa bunge hilo.

Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu.

Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post