Sakata la ushoga!! SHOGA ACHOMWA MOTO HADI KUFA HUKO UGANDA


Ni muda mfupi tu toka Uganda ipitishe sharia ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto mpaka kufa nchini humo.

CNN imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu (KULIA PICHANI) huyo halikuweza kujulikana. 
 
Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku akiwa pembeni mwa reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
 
Sheria hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha pamoja na kufungwa maisha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za ushoga pamoja na kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.


Sharia hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha “Ua Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa matendo fulani ya ushoga, lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi zilizopigwa na mataifa mbalimbali.
 
Katika sheria hii mpya, mtu yeyote atakaye fungisha ndoa ya jinsia moja atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 7. Atakayeshindwa kutoa taarifa ya ushoga polisi pia ni muharifu.
 
Madaktari watakao watibu mashoga, watakaopangisha mashoga kwenye nyumba zao na wale wataka shukiwa kuwa mashoga, wasagaji, waliobadilisha jinsia na mabasha watafungwa miaka 5.
 
Mtu yeyote atakayetoa msaidia kwa shoga atakuwa anavunja sharia, ambapo atachukuliwa hatua.
 
Watu wengi wanaamini kuwa sharia hii ni muhimu ili kupinga tabia na tamaduni za nchi za magharibi.
 
 “ hii sharia ni muhimu kwa nchi hii ili kulinda tamaduni za Mwafrika” alisema David Bahati ambaye ni mbunge ambaye aliuwakilisha muswada huo bungeni.
 
Bahati pia ni mmoja kati ya kundi linalotuma fedha katika nchi za Afrika kuunga mkono wanaopinga shughuli zote za ushoga.
 CREDIT - USWAZI24

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post