OSTAZ JUMA ASEMA PNC ANAHARIBIWA NA BANGI NA UGORO,PNC NAYE ATEMA CHECHE SIKILIZA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQ5P0NL5qKu240J65GRGJf-F9ONlTaqXVyCP-32BnpHC5LxnsxKEtibxrB4g5yoniBlQbJMnhhiZascWtISbIFkswE_TeEvlDtlafK1JVK654C7botyX-t9N9ZCKVyMDhlBAzFXSYw6xw/s1600/ostaz+juma+na+musoma.jpgWakati ambapo Mashabiki wa Msanii PNC wakijiuliza maswali kuwa Msanii huyo ataendelea kufanya kazi chini Ostaz Juma na Musoma Kupitia Kampuni ya Mtanashati Entertainment. PNC ametangaza wazi kuwa amejitoa chini ya Label hiyo.


Akipiga Story na DjHaaazu ndani ya MJ FM Arusha kupitia kipindi cha DUNDO PNC amesema ameamuia kujitoa chini ya Mtanashati kwa kile ambacho amekisema kuwa amegundua wazi kuwa ni kweli ile picha iliyosambazwa kwenye mitandao ikimuonyesha akimpigia Magoti Ostaz ni kweli ilipigwa na mdogo wa Ostazi Juma aitwaye Faraji ila mtu wa kwanza kuipost kwenye mitandao ni Ostaadhi Juma mwenyewe akitaka kumuharibia PNC.
PNC amefunguka kuwa hata mashabiki wake hawapo tayari kumuona akiendelea kufanya kazi na Mtanashati hivyo ameamua kufanya kazi kivyake.
Kufuatia interview hiyoilibidi DjHaazu kuutafuta upande wa pili ambapo aliamua kumvutia wire Ostaz Juma na Musoma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjcusGqRayWb6BIVgqbjd57hoDWKtGUs2-zySDoWLWUHaXVvuRehCuouE40hwtUKvr5_q-zzpjhvXEiiT9HAKoIoivhpWZd9IHjdFwBg7ut_3331VihvupCZJ3xZTpsel2sIDn3lBInHg/s1600/Screenshot_2014-02-27-11-36-49.png
Ostaz alianza kusema PNC bado yuko Mtanashati na ndio maana alimlipia Kurecord wimbo kwa Mazuu na kuisimamia kwa kutoa mpunga wa Maana kwa ajili ya Promotion ya wimbo huo ambao ni SINA MAKOSA ukiwa ni wimbo Mpya wa PNC wimbo ambao PNC ameutoa kwa ajili ya kuwaambia mafans wake hana makosa kuomba msamaha pale anapohisi amekosea.
Ilikuwa Suprise kwa Ostaz juma kuambiwa na Haazu kuwa PNC amejitoa Mtanashati na ndipo Ostaz alipoanza kumchafulia jina PNC redioni kuwa PNC anavuta bangi na kula ugoro na kusisitiza kuwa anayoyaongea ni kweli. Cha kushangaza zaidi ni pale aliposema kuwa PNC hawezi kusurvive bila yeye kwani anamlisha na kumvisha PNC na Mkewe hivyo bila yeye hawawezi.
MSIKILIZE HAPA CHINI PNC AKIZUNGUMZA NA DJ HAAZU

MSIKILIZE HAPA CHINI OSTAZ JUMA AKIMPONDA PNC NA KUHUSU JAMAA KULA BANGI NA UGORO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post