Nouma kweliii!! MWANAMKE AHUKUMIWA MIAKA 7 JELA KWA KUIBA MTOTO HUKO GEITA

Mahakama  ya wilaya ya Geita mkoani Geita imemhukumu Joyce Charles(25) mkazi wa mtaa wa bomani mjini hapa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuiba mtoto Godfrey Arbet(2) aliyekuwa amemsubiri mama yake nje ya geti kwa ajili ya kwenda kanisani siku ya krismas mwaka jana.

Hakimu wa mahakama hiyo Zabron Kesase alielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo siku ya tar25 desember mwaka jana mnamo saa 4 asubuhi katika mtaa wa ihayabuyaga mjini hapa ambapom mama huyo wa mtoto aliyekuwa anajiandaa kwenda kanisani na mtoto wake mara baada ya kumaliza kumuandaa na ili waondoke ghafla alitokea mama huyo na kumbeba na kuenda nae hadi eneo la mtaa wa kagera kabla hajakamatwa na wananchi.

Mwendesha mashitaka wa serikali Fredi Jairo alidai mahakamani kuwa mtuhumiwa siku ya tukio hilo alimuiba mtoto huyo na kutokomea kusikojulikana huku akidai kuwa mtoto alimlilia ndio maana akamchukua na kuenda naye na hata hivyo baada ya mama wa mtoto kubaini kuwa ameibiwa mtoto akatoa taarifa sehemu mbalimbali kwa wananchi na hatimaye kumkamata mtuhumiwa huyo.

Baada ya kukamatwa alipelekwa kituo cha polisi ambapo baadaye alipelekwa mahakamani kwa kitendo alichokifanaya ambapo kamanda wa polisi Leonard Paul alithibitisha kwa tukio hilo kwa ni alifika kwenye eneo la tukio na kujionea mazingira ya mtoto huyo kibiwa.

Hata hivyo baada ya kuridhika na ushaidi uliotolewa na upande wa mashitaka mahakama ilimtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka saba kabla ya kujitetea mbele ya mahakama na kupunguziwa adhabu ya miaka mitano kwenda jela ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutaka kutenda makosa ya namna hiyo.
 
Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post