MTOTO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHINJWA NA BABA YAKE HUKO KAHAMA,KISA KUUGUA MUDA MREFU

Mtoto Said Siraji akiwa amelazwa katika Hospital ya wilaya ya Kahama
Matukio ya kikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mtoto aitwaye Said Siraji/Said Joshua  amelazwa katika Hospitali ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio la kuchinjwa na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Salvatory. 

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya-Kahama; Dakta Joseph Fwoma amesema Siraji amefikishwa hospitalini hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huko akivuja damu shingoni.


Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwisha achana siku nyingi.

Mariam amesema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Siraji mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya.
 
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post