MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NA BABA YAKE HUKO KAHAMA AFARIKI DUNIA

Mtoto Said Joshua enzi za uhai wake akiwa amelazwa hospitalini baada ya kukatwa shingo na Baba yake

Mtoto Said Joshua (12), mkazi Majengo Kaskazini wilayani Kahama mkoani Shinyanga aliyedaiwa kukatwa shingo na baba yake  usiku wa kuamkia Machi nne mwaka huu, amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazin Noel Makula Museven amesema mtoto huyo aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Majengo wilayani Kahama amefariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post