MESSI WA SIMBA AVUNJA MLANGO UWANJA WA TAIFA YADAIWA PENGINE SABABU ZA KIPIGO CHA COASTAL UNION

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anadaiwa kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Wakundu wa Msimbazi wakifungwa 1-0.

Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.

Polisi walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa. 

Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
CREDIT:BIN ZUBEIRY

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post