Mauaji!! KIJANA AUA BIBI YAKE KWA JEMBE,WANANCHI WAMGEUKIA NA KUMPA KIPIGO HADI KUFA

Kijana mmoja mkazi wa Kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi,mkoani Tanga Hassani Said (28) amemuua kwa kumkata na jembe kichwani bibi yake, lakini baadaye akauawa na wananchi wa eneo hilo.

Mkazi mmoja wa kijiji hicho Omari Waziri alisema kuwa Februari 25 mwaka huu kijana huyo alikuwa akitoka shamba na bibi yake aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Waziri (62), lakini ghafla alinyanyua jembe alilobeba na kumkata kichwani bibi yake na kufariki dunia.
Alisema kuwa baada ya kufanya mauaji hayo, Hassan alijificha kwenye nyumba iliyo jirani na wananchi walipopata taarifa akiwemo babu yake, Mkomwa Mkombozi (72) walikwenda kwa lengo la kumkamata.
Katika jitihada za kumkamata, mtuhumiwa alitoa panga na kumjeruhi vibaya Mkombozi ambaye anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Handeni.
Baada ya kumtia mikononi, wananchi walimshambulia kwa zana mbalimbali hadi kumuua.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa, mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alipotafutwa na kuhusu tukio hilo, alisema hafahamu lolote kwa vile yuko nje ya ofisi.
Chanzo-Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post