MAJI YAVUNJA NDOA PEMBEZONI MWA ZIWA TANGANYIKA,SOMA ZAIDI HAPA

Imefahamika kuwa,Ukosefu wa Maji kwa wakazi wa Mwambao wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma limekuwa sugu ,hali inayosababishia wanawake  wanaoishi katika vijiji  husika  kuvunjika kwa ndoa  zao .

Changamoto hiyo inayowakabili wakazi hao inatokana na viongozi husika kutokuwajibika ingawa vijiji hivyo vipo pembezoni mwa ziwa Tanganyika hali inayochangia jamii iwe sehemu ya uchafuzi wa mazingira ya ziwa hilo lenye rasilimali ya madini ya gesi,samaki ,dagaa wa aina mbalimbali.

Mkazi wa Kalalangabo,  Kabwe  Mzee alisema  kumekuwa na mgogoro wa mahusiano  hasi kati ya mke na mume kwa kuwekeana dhana potofu kuwa huenda mkewe hakuwa kisimani kusubiri maji na hivyo kupelekea ndoa zao kuvunjika.

“kuna korongo moja ambalo kijiji kinategemea maji ya kunywa na kupikia sasa nyakati ya kiangazi hali huwa mbaya zaidi kutokana na foleni kubwa kina mama huamka alfajiri kuwahi foleni hapo sasa baba haelewi kama si kichapo ni kumtanga talaka tu” alidai Mzee.

Mwatano Shaban  na Sophia Steven  Mkazi wa Ilagala  alisema wanawake wamekuwa wahanga wa changamoto hiyo kutokana na wanaume kutojali umbali wa eneo la maji safi na wingi wa hitaji kwa wakazi husika, wanachojua wao ni kutoa adhabu ya kipigo na talaka hali inayosababisha watoto waishi maisha hatarishi.

Diwani wa kata ya Kalalangabo, Maganga Patrick alisema awali kata ilikuwa na bomba eneo la kolongo  ni mita 100 kutoka kijijini hapo, lakini liliharibika kitambo hali inayowalazimu  kusubiri  foleni kisimani na wanaume wasio na uelewa wa mambo huwapa talaka wake zao hatimaye watoto wanakosa mapenzi ya wazazi wawili.

Makem Shaban na Maria Joackim wakazi wa kata ya Kalya kwa nyakati tofauti walisema serikali imeshindwa kuwajibika kwa wazi wa mawambao wa ziwa Tanganyika na wamekuwa wakiwatumia nyakati za uchaguzi ili kutimiza ndoto zao na si kutatua kero za wananchi wake hali inayochangia wakazi  wa mwambao wa ziwa hilo kuwa nyuma ki maendeleo.

Wakatihuohuo Chama cha wandishi wanawake Nchini wanaendeleza kampeni ya kuishinikiza serikali itambue madhara ya GBV  yanachangia kuzorota kwa maendeleo ya jamii husika,huku Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila alidai changamoto za maji na miundombinu kwa wakazi wa jimbo lake litakwisha mwishoni mwa mwaka huu.
 
 Na  Magreth Magosso-Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post