FUATILIA HAPA TUKIO LA UZINDUZI WA WIKI YA MAJI DUNIANI,MKOANI SHINYANGA WAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA BUBINZA WILAYANI KISHAPU,MKUU WA MKOA AONGOZA ZOEZI ZIMA


Uzinduzi wa wiki ya maji Duniani katika mkoa wa Shinyanga.Hapa ni katika eneo la mradi wa maji katika kijiji cha Bubinza kata ya Mwamashele wilayani Kishapu,mradi ambao umetajwa kuwa utanufaisha  wananchi zaidi ya elfu nne wa kijiji hicho,chanzo cha maji hayo ni mto Tungu,na pembeni mwa mto huo kumechimbwa visima virefu,kutakuwa na vituo 15 vya kuchotea maji,matanki 3 na vituo vya kunyweshea mifugo viwili.Ni kaimu afisa mtendaji wa kijiji cha Bubinza kata ya Mwamashele wilayani Kishapu bwana Luhende Njungu akisoma risala kuhusu mradi huo wa maji ambao unajengwa na kampuni ya “NAMRAMBA BLOCK X CONTRACTOR” kwa  kushirikiana na kampuni ya ushauri NEFWAS LTD.Bwana Njungu alisema mradi huo umenza mwaka jana na unatarajiwa kukamilika mwezi huu ili kuondoa changamoto ya wanakijiji hao kutumia muda mwingi kufuata maji katika mto Tungu ambao uko umbali wa takribani kilometa 4.3.

 Ni katika eneo la mradi wa maji kijiji cha Bubinza kata ya Mwamashele wilayani Kishapu leo,ambapo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga leo amezindua wiki ya maji duniani ki mkoa katika kijiji cha Bubinza kilichopo kata ya Mwamashele wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,akiwa katika kijiji hicho ,ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji katika kijiji hicho,mradi ambao umegharimu zaidi shilingi milioni mia tano na kati ya hizo shilingi milioni 12 zinatokana na mchango wa wananchi wa kijiji hicho ambapo kaya zaidi ya 500 zimechangia shilingi elfu 25 ili kufanikisha mradi huo wa maji ambapo chanzo chake kikuu ni Mto Tungu uliopo wilayani Kishapu.Kikundi cha  Makhirikhiri kutoka kijiji cha  Bulimba kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu ambacho kwa sasa ni maarufu sana kwa burudani kikimpokea mkuu wa mkoa katika eneo la mkutano wa hadhara katika kijiji cha Bubinza wilayani Kishapu.
 


Mwenye suti ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku baada ya mzuka kupanda akavunja ukimya na kuamua kucheza ngoma ya Makhirikhiri kutoka kijiji cha Bulimba kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga ili azungumze na wananchi wa kijiji cha Bubinza ambako leo kumefanyika uzinduzi wa wiki ya maji duniani.Pamoja na mambo mengine mkuu huyo wa wilaya aliushukuru uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuchagua wilaya ya Kishapu kati ya halmashauri 6 za mkoa  kuwa mwenyeji wa siku ya uzinduzi wa wiki ya maji kimkoa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga  kabla ya hotuba yake akikabidhi pesa  jumla ya shilingi elfu 80 kwa kikundi cha Burudani cha MakhiriKhiri.a(kiongozi wao anapokea)Hii ni  baada ya kufurahishwa na kazi yao,wageni mbalimbali walioambatana na mkuu wa mkoa wakakusanya kile walichokuwa nacho kwenye mifuko yao kwa ajili ya kuwapongeza vijana hao ambao kiukweli wanajua wanachokifanya mithili ya makhirikhiri wa nchini Botswana.
 Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika uzinduzi huo
Aliyesimama ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza na wananchi wa kijiji ch Bubinza ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watunze mradi huo huku akisisitiza wananchi katika halmashauri zote za wilaya katika mkoa wa Shinyanga kupanda miti katika maeneo yanayozunguka miradi ya maji ili kutunza uoto wa asili
Mkuu wa mkoa (mwenye suti nyeusi upande wa kulia)akitoa hotuba yake katika kijiji cha Bubinza wilayani Kishapu

Baada ya hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Makhirikhiri wakaendelea kufanya yao
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika eneo la tukio
Wageni mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara za ulinzi na usalama mkoani Shinyanga wakiangalia kikundi cha Makhirikhiri.

Katika kuadhimisha wiki ya maji kesho tarehe 16 kutakuwa na uzinduzi wa mradi wa maji wa Mwamalili/Seseko katika manispaa ya Shinyanga,Machi 18 katika kijiji cha Bulekela wilayani Kishapu,Machi 19 kijiji cha Mwamashele manispaa ya Shinyanga,Machi kijiji cha Mishepo wilaya ya Shinyanga,Machi 21 kijiji cha Ibadakuli,Nhelegani katika manispaa ya Shinyanga na Machi siku ya kilele cha wiki ya maji ni katika kijiji cha Kagongwa/Iponya ambapo mbali na kuzindua miradi katika vijiji hivyo pia kutafanyika mikutano ya hadhara sambamba na kuhamasisha wananchi(elimu kuhusu umuhimu wa kuchangia fedha kwa ajili ya mfuko wa maji)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post