Kali ya mwaka !!! KIJANA ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMLAWITI KIJANA MWENZAKE BAADA YA KUMNYWESHA POMBE YA KIENYEJI

Nb-picha haiendani na habari
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu  Wiliamu  George 32 Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa  Wilaya ya Mpanda  kifungo cha miaka  30  jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti  kijana mwenzie  22 Mkazi wa Mtaa wa Mpandahoteli baada ya kumnywesha pombe ya kienyeji kupita kiasi.
 
Hukumu  hiyo  ilitolewa  hapo  jana  na  Hakimu  mkazi   mfawidhi wa  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga  Ntengwa   na hukumu  hiyo   kuvuta hisia za watu mbalimbali  wa  maeneo ya mji wa Mpanda na Mkoa wa Katavi.
 
Hukumu  hiyo ilitolewa na Hakimu wa mahakama hiyo  baada ya  mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa  mahakamani hapo wa   upande wa mashitaka na upande wa utetezi.
 
Katika kesi hiyo hapo awali mwendesha mashitaka mkaguzi wa jeshi la polisi Ally Mbwijo  alidai mahakamani hapo kuwa  mshitakiwa  alitenda kosa hilo hapo Novemba  21 mwaka jana   majira ya kumi na mbili jioni  katika mtaa wa Mpanda Hotel.
 
Mshitakiwa  siku  hiyo ya tukio kabla ya kutenda  kosa  hilo la kumlawiti kijana  huyo alidaiwa  kunywesha pombe  ya kienyeji aina ya komoni , walikuwa wakichanganya na bia  nyumbani kwa mwanamke  aliyekuwa akiwauzia pombe aliyetambulika kwa jina moja la Lita katika mtaa huo wa Mpanda hotel.
 
Ilielezwa na mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alisema kuwa  mshitakiwa  baada ya kuona mwenzake  anatoka  anatoka nje kwenda kujisaidia  alimwagiza dukani  Lita  aende akamnulie  sigara.
 
Alieleza mahakama baada ya  kijana  huyo amba ejina lake limehifadhiwa  kurudi  ndani  aliendelea na kunywa pombe ambayo alikuwa ameishaiweka kwenye chupa yake na  ndipo alipoteza fahamu na mshitakiwa alitumia nafasi huyo kumwingilia  kinyume cha maumbile yake huku akiwa amemlaza kwenye kochi.
 
Mwendesha  mashitaka  alieleza  Lita  alipotoka  dukani  alimkuta  mshitakiwa akiwa amekaa karibu na kijana huyo  ambae alikuwa  amevuliwa nguo yake  ya saruali  na akiwa hajitambui na sehemu zake za  matakoni zikiwa    na mbegu za kiume.
 
Mshitakiwa  baada ya kufanya kitendo hicho  siku iliyofuata  alimtuma  mama yake mzazi aende  kwa kijana huyo akamwombee samahani  kwa kile alichoeleza kuwa anahofia  kufungwa jela.
 
Baada ya mama mshitakiwa  Wiliamu  George  kumwombea msamaha kwa kijana aliyelawitiwa  alikubali  kumsamehe  mshitakiwa  kwa kuhofia  kupata aibu.
 
Mshitakiwa baada ya kusamehewa  alianza kumtangaza  kijana huyo  kwa rafiki zake  na  kuwafahamisha kuwa kijana huyo ni shemeji yao  kitendo ambacho kilimkasirisha kijana huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kulawitiwa  kwake na Mshitakiwa Wiliamu George.
 
Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga Ntengwa kabla ya kutoa hukumu hiyo  aliiambia mahakama kuwa  mahakama imemtia hatiani mshitakiwa  Wiliamu  George kwa kosa la kumwingilia  kijana huyo  kinyume na maumbile yake hivyo mahakama inatoa nafasi kwa mshitakiwa kama anasababu ya msingi ya kuishawishi mahakama impunguzie  adhabu  aieleza mahakama  hiyo.
 
Katika utetezi wake mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwani  yeye hakutenda kosa hilo na pia umri wake bado ni kijana mdogo na wazazi wake bado wanamtegemea  maombi ambayo yalipingwa vikari na mwendesha mashitaka.
 
Hakimu Chiganga baada ya  kusikiliza  utetezi huo aliiambia mahakama kuwa  mshitakiwa amehukumiwa na  mahakama  baada ya  kupatikana   na hatia ya kumwingilia kinyume na maumbile kijana huyo na  anahukumiwa na adhabu ya kifungu cha sheria  namba  235 sura ya 20 ya mwaka 2009 hivyo Wiliamu George mahakama imehukumu kutumikia jela kuanzia jana kifungo cha miaka 30 jela.
 
Na  Walter Mguluchuma-Mpanda Katavi
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post