ITV ,STAR TV NA RADIO FREE AFRICA VYANUSURIKA KUFUNGIWA,WAPEWA ONYO KALI NA TCRA

Na Karoli Vinsent
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imevipa onyo kali Itv na Startv pamoja na RadioFree,kutokana na kurusha Tangazo ambalo linakwenda kinyume na Maadili,Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano na Waandishi wa Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka hiyo,Margaret Mnyagi ambapo alisema Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kushauriana na Kamati Maudhui ya vipindi vya Runinga vya mamlaka hiyo. 

“Tumefika maamuzi haya baada ya kukaa sisi kama kamati ya Maudhui na kubaini tangazo la Policy Forum ambalo tangazo hilo linachochoe watu wasilipekodi,Tangazo hilo lilirushwa kwenye Runinga mbili ambazo ni Itv pamoja na Startv na redio ambayo ni Radio Free”


“Napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa atuchafanya upendeleo wowote katika kutoa hukumu hii”alisema Mnyagi


Aidha Mamlaka hiyo imevitaka vyombo hivyo vilivyorusha Tangazo hilo viwasilishe mwongozo wa urushaji wa Matangazo hayo,na pia Mamlaka hiyo imevionya vyombo hivyo kutorudia kuonyesha Matangazo ya Uchochezi,na endapo watakaidfi Mamlaka hiyo itawachukulia hatua kali za kisheria.


Kwa upande wake Meneja wa Mipango na Utafiti wa Sahara media Nassani Lwehabula ambao ni wamiliki wa Startv,kissfm,Radio free,Gazeti la Msanii wa Afrika alisema wao wamechukulia Hukumu hiyo ni kama Changamoto kwao ya kufanya Vipindi vyao kwa umakini ili waweze kukuza maudhui yao,

Ikumbukwe Tangazo liloifanya Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuchukua Maamuzi hayo ni Tangazo la Taasisi isiyokuwa ya kiSerikali inayojulika PolcyForum,ambapo katika Tangazo hilo linawahamasisha wananchi wasilipe 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post