Hatari!! DIWANI NA AFISA MTENDAJI WANUSURIKA KUCHOMWA MOTO HUKO IGUNGA

NB-Picha haiendani na habari hapa chini
Diwani wa Isakamaliwa, Igunga, Doto Kwilasa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Erasto Shokoro, wajumbe sita wa serikali ya kijiji na mtu ambaye hajajulikana wamenusurika kuchomwa moto na wananchi.
 
Wananchi hao waliwafungia ndani ya chumba cha mikutano viongozi hao kwa madai ya kuitisha kikao cha kuwazuia vijana wa Isakamaliwa wasilipize kisasi kwa wafugaji waliowachoma mikuki vijana wenzao.
 
Vurugu za kutaka kuchoma moto chumba hicho zilitokea juzi katika Kijiji cha Isakamaliwa baada ya makundi mawili ya wafugaji wa kata hiyo kutofautiana na kusababisha kundi moja kushambulia jingine kwa mikuki wakidaiwa kuingiza mifugo kinyume cha sheria katika bonde la Magogo.
Chanzo;Tanzania Daima

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post