Hakuna Mchezo!!! WANANCHI WAVAMIA NYUMBANI KWA AFISA MTENDAJI NA KUMTAKA AHAME MARA MOJA KISA HAJAFANYA LOLOTE TANGU AHAMIE KWENYE KIJIJI CHAO




HUYU NI MTENDAJI WA KIJIJI HICHO BWANA BATISTA MSEMWA AKIWA NDANI YA NYUMBA YAKE HUKU WANANCHI WAKIWA NJE KWA NIA YA KUMFUNGASHIA MALI ZAKE NA KUMPELEKA KATIKA OFISI YA KATA YA MDANDU.




Wananchi wa Kijiji cha Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe jana Walitoa Muda wa Saa Mbili Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Bwana Batista Msemwa Kuhama Kijijini Hapo Kwa Madai Ya Kuwa Tangu Alipohamia Kikazi Kijijini Hapo Hakuna Kazi Alizozifanya.

Mapema Leo Wananchi Hao Walikusanyika Nyumbani Kwa Afisa Mtendaji Huyo Wakimtaka Aondoke Haraka Iwezekanavyo Kabla Ya Wao Kuchukua Maamuzi Magumu ya Kumuondoa Kwa Nguvu Kwa Madai ya Kuwa Tangu Ahamishiwe Kijijini Hapo Hakuna Kazi Alizozifanya Kwa Kuwa Walishamkataa Tangu Awali.

Kumkataa Afisa Mtendaji Huyo Kulitokana na Kile Kinachodaiwa Alisikika Kwenye Vyombo Vya Habari Kuwa Anatuhumiwa Kufuja Mali za Kijiji cha Itambo Hivyo Tangu Serikali Imuhamishie Kijijini Hapo Wananchi Walimkataa Mbele ya Afisa Mtendaji wa Kata na Diwani Kitu Ambacho Hadi Sasa Bado Ameendelea Kuwepo Kijijini Hapo Bila Kazi Yoyote,Na Hapa Wananchi Hao Wanasema.

  Mwandishi wetu amefanikiwa Kuzungumza na Afisa Mtendaji Huyo Bwana Batista Msemwa Ambaye Amekubali Kuondoka Kijijini Hapo Huku Akakanusha Tuhuma za Wananchi Hao

Tangu Mwezi Septemba Mwaka Jana Wananchi Hao Walipo Muondoa Madarakani Mwenyekiti wa Kijiji Hicho na Kumkaimisha Bwana Shaibu Mahegele Ndipo Walipomkataa na Afisa Mtendaji Huyo Ambaye Aliendelea Kuishi Kijijini Hapo Bila Kufanya Kazi za Kijiji.

Hali Hiyo Imetajwa Kusababisha Uhalifu na Wizi Mkubwa Kijijini Hapo Kutokana na Kukosekana Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Ambaye ni Msimamizi wa Amani Kijijini Hapo..
  Na  Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post