MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WILAYA YA SHINYANGA YAFANYIKA KATA YA KIZUMBI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akiangalia baadhi ya bidhaa za wajasiriamlai wanawake kutoka katika manispaa ya Shinyanga wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nhelegani katika kata ya Kizumbi iliyopo katika manispaa ya Shinyanga.
Bidhaa za wajariliamali wanawake katika manispaa ya Shinyanga zikiwa eneo la sherehe za siku ya wanawake duniani katika wilaya ya Shinyanga,bidhaa zingine zilizotengenezwa na wajasiriamali hao ni pamoja na sabuni za aina mbalimbali,mashuka,vitambaa,vitu vya asili n.k
Aliyesimama ni mgeni rasmi wakati wa maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Anna rose Nyamubi akitoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine alisema ukosefu wa huduma muhimu za kijamii kama vile vituo vya afya na maji  ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake waishio vijijini hali inayochangia kwa kiasi kikubwa wanawake kuendelea kunyanyasika kijinsia katika jamii na kuongeza kuwa akina mama wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta huduma hizo na hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo na kubaki kuwa tegemezi kwa waume zao hali ambayo huchangia wanawake kuendelea kukandamizwa.Mkuu huyo wa wilaya akatumia fursa hiyo kuziagiza halmashauri za wilaya katika wilaya yake kuwa zinatenga pesa kila mwaka ambazo
zitasaidia kujenga miundombinu katika jamii hasa kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini kwa kuwaekea miradi ya maji na kuboresha huduma za afya.
Michezo mbalimabli ilikuwepo katika sherehe hizo kama vile uvutaji wa kamba.Katika hotuba yake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna rose Nyamubi pia alizungumzia suala la mauaji ya vikongwe ambapo asilimia kubwa ya wahanga ni wanawake ambapo aliitaka jamii kubadilika na kukumbuka kuwa  kila mtu ni mzee mtarajiwa huku asisitiza kuwa vitendo vya kuua ndugu zetu ni ukiukwaji wa haki za binadamu  na ni kumkosea mwenyezi mungu akawaomba wananchi kushirikiana na  viongozi wa vitongoji,vijiji,tarafa, kata, wilaya kuwafichua wahusika wa mauaji hayo ili  jamii ya Shinyanga iishi kwa amani ,utulivu na upendo.PICHA ZOTE NA MARCO MADUHU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post