Majanga tena Geita!!! NYUMBA ZACHOMWA MOTO KWA USHIRIKINA,DC AGEUKA MBOGO

NB-picha haiendani na habari hapa chini
Ikiwa ni takribani wiki moja imepita  baada ya kaya 5 katika kijiji cha Kakeneno kata ya Buziku wilayani Chato kuchomwa  moto na wananchi kwa kisingizio cha kwamba wamiliki wake ni wachawi katika hali ya kushangaza vitendo hivyo vimezidi kujitokeza safari hii ni katika  kijiji cha kilombero 2 ambapo kaya 7 zimeteketezwa kwa moto Februari 15 mwaka huu.

Kitendo hicho kinachohusishwa na imani za kishirikina kimezua tafrani katika  kijiji hicho na kimesababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo kutoroka na kukimbia kusikojulikana.


Chanzo cha tukio la kuchomwa moto nyumba hizo kumetokana na tukio la mwanamke mmoja aitwaye Felister Mathias kuuawa kwa kukatwa katwa mapanga mwanzoni mwa mwezi huu.

Akizungumzia kuhusu chanzo cha tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji  cha kilombero 2 Matiba alisema kuwa mama huyo inadaiwa kuwa mifugo yake iliingia kwenye shamba la jirani yake na baada ya hapo wakapelekana kwenye vyombo vya sheria na mama huyo akakiri kulipa kisheria.

“Cha kushangaza baada ya muda mlipwaji(jirani) alikataa kumlipa kisheria na alitaka amlipe kimya kimya lakini mama huyo alikataa na kabla ya siku waliyoahidiana kulipa mama huyo alikatwakatwa mapanga huku wakidhani kuwa ni mshirikina”,alieeleza afisa mtendaji.

Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo baadhi ya watu waliokamatwa na jeshi la polisi wakihusishwa na tukio hilo walipelekwa kituoni .

“Kufuatia kukamatwa kwa wanachi,baadahi ya wananchi waliosalia  walihisi kuna watu wamesababisha wenzao kukamatwa wakaanza kualikana na kuanza kuchoma nyumba baadhi ya kaya walizokuwa wanadhani ni chanzo cha mgogoro huo tarehe 15 mwezi huu”,aliongeza.

Kwa upande wa diwani wa kata ya Rwamgasa kilipo kijiji hicho Christopher Kadeo alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema kuwa hajui kama kuna kitu cha namna hiyo.

Kwa upande wa katibu wa shirika lisilo la kiserikali  linalotoa msaada wa kisheria  na haki za binadamu wilayani Geita Elineema Charles alisema ni vyema vitendo hivi vikakemewa na jamii pamoja na serikali kwani vimekuwa vikijirudia mara kwa mara. 


Baadhi ya kaya zilizochomwa ni pamoja na familia ya Hamis Kisumo,kisumo sama,Elias Kisumo,Shija sahani,Luka Ngodagula,Orogwe Kisumo ambaye ni mtemi wa sungusungu, na India Sahani, Will itenga huku baadhi yao wakiwa wamekimbia makazi yao.


Kufuatia kuchomwa kwa kaya hizo 7 mkuu  wa wilaya ya Geita Manzie Omari Mangochie mkoani Geita ametoa siku kumi kwa viongozi wa kijiji cha kilombero 2 kuhakikisha wanawatafuta na kuwakamata watuhumiwa kwa namna yoyote kwani hapo kijijini wanajuana tabia zao.

Mkuu huyo ametoa agizo hilo mapema juzi mara baada ya kutembelea kaya saba zilizochomwa moto na wananchi wenye hasira kali kutokana na chanzo chake kikiwa ni imani za kishirikina.

Imeelezwa kuwa kijiji hicho matukio ya namna hiyo yanatokea sana ambapo hilo ni tukio la 5 katika muda wa miezi 12.

Na Valence Robert-Geita


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post