Ni balaaaa!!! FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA LA MKUTANO MKUBWA WA WAFANYABIASHARA WA SHINYANGA NA MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU ULIOFANYIKA LEO MJINI SHINYANGA




Awali meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga bwana Philbert Rweyemamu akizungumza leo katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga katika mkutano wa wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,mkutano ambao umeandaliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu African Barrick ukiwa na malengo mbalimbali kama vile mpango wa migodi hiyo wa kendeleza wagavi wa ndani ya nchini.Mpngo huo unalenga kuongeza idadi ya wagavi,kuongeza ukubwa wa biashara inayofanyika,kuongeza idadi ya bidhaa na huduma zinazonunuliwa katika maeneo husika au yote.Lakini pia mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa ndani ili waweze kufikia viwango vinavyotakiwa na African Barrick Gold Mine katika muda maalum sambamba na kuwaendeleza wafanyabiashara waliopo na kuwapa nafasi wapya


Aliyesemama ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo wa kwanza kuwakutanisha wafanyabiashara mkoani Shinyanga na migodi ya madini, akitoa salamu zake kwa wafanyabiashara hao ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka watumie fursa ya migodi hiyo kuinuia uchumi wa mkoa ambapo kwa sasa kipaumbele chake ni sekta ya madini,Kilimo na viwanda vilivyopo na vinavyoendelea kujengwa mkoani humo
Kulia ni meneja wa Kampuni ya African Barrick mahusiano ya jamii bwana Steve Kisyake akifurahia maneno mazuri ya Mkuu wa mkoa(aliyesimama) kwa wafanyabiashara mkoani Shinyanga ambapo mkuu huyo wa mkoa Ally Nassoro Rufunga pamoja na mambo mengine  alisema serikali itaendelea kushirikiana na migodi katika shughuli mbalimbali huku akiwataka wafanyabiashara kufika katika ofisi za mkoa kama wanapata matatizo na kuongeza kuwa sekta ya madini ni miongoni mwa  sekta zinazotemewa kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi wa mkoa wa Shinyanga.
Kushoto aliyesimama ni meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (muafrika wa kwanza)uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga bwana Philbert Rweyemamu akizungumza baada ya hotuba ya mkuu wa mkoa ambapo meneja huyo mzawa,alisema kampuni yake inalenga katika kushirikiana na wafanyabiashara wa ndani kuendeleza uchumi wa nchi na kutoa fursa katika ngazi ya jamii za kujishughulisha katika biashara kwa kuwapa kipaumbele zaidi wagavi wa ndani.
Aidha  alisema ununuzi wa ndani utasaidia katika kupunguza thamani ya bidhaa zinazohifadhiwa kwa wingi na kuongeza mzunguko wa fedha katika kufanya uwekezaji kwenye miradi mingine huku akiahidi migodi hiyo kuendelea kukutana na wafanyabiashara kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kibiashara ili kuendana na kauli mbiu ya mkoa aliyoianzisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga bwana Rufunga inayosema "SHINYANGA UCHUMI IMARA"
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambapo alisema ofisi yake inatambua malalamiko  mengi ya wafanyabiashara kuhusu kutopewa fursa ya kufanya biashara na migodi hiyo jambo ambalo limekuwa likikwamisha ukuaji wa biashara zao,hivyo akatoa wito kwao kufanya biashara na migodi kwa kuwauzia bidhaa mbalimbali kwani migodi hiyo haibagui mtu, lakini akawaasa kufanya biashara kwa kuzingatiaa sheria na taratibu za biashara na za nchi.

Mapema meneja Ugavi  nchini kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick(ABG) Dickson Luwumba(aliyesimama) akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema mkoa wa Shinyanga una takribani wagavi 40 na kuongeza kuwa pamoja na kampuni hiyo kutobagua watu wakufanya nao biashara lakini wafanyabiashara walioko katika maeneo ya migodi wanapewa kipaumbele zaidi.Meneja huyo 
alivitaja vigezo vya kufanya kazi na kampuni hiyo kuwa ni wagavi hao kuwa na vibali vya biashara,uwezo wa kibiashara,jengo au ofisi ya biashara,kuwa na bidhaa anazouza na kuwa wakala aliyeidhinishwa
Meneja Ugavi  nchini kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick(ABG) Dickson Luwumba aliyesimama alisema miongozni mwa changamoto zilizopo sasa ni wafanyabiashara wazalendo kushindwa kuonyesha uwezo wao katika biashara,kushindwa kutoa majibu ya haraka kuhusu bei na upatikanaji wa bidhaa au huduma lakini pia hakuna ushirikiano miongoni mwa wafanyabiashara,wengi wanaendekeza majungu na ushindani usio na mtazamo wa kibiashara
Maafisa mbalimbali kutoka mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (Wa kwanza kushoto ni afisa uhusiano  mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Bi Blandina Mughezi)wakifuatilia mawilia matatu yaliyokuwa yanajili katika ukumbi wa mikutano wa Karena Hoteli mjini Shinyanga


Mkutano unaendelea ambapo kampuni hiyo ya uchimbaji madini imekuja na mpango wa kushirikiana na wafanyabiashara wa ndani ili kuinua uchumi wa nchi pamoja na kwamba wafanyabiashara wengi kuridhika na kutotaka kubadilika na wengi wao kuendesha biashara bila kufuata misingi ya sheria,taratibu na kiwango cha juu cha maadili
Mkutano uanendelea ambapo masuala kadha wa kadha yalijadiliwa na lengo kuu ni migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuwa wanayo fursa ya kufanya biashara na migodi hiyo huku wafanyabiashara hao wakiaswa kuwa tayari kushirikiana na migodi hiyo ambayo inaendelea kujitahidi kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayoishi karibu na migodi hiyo
Katika mkutano huo wa kihistoria katika mkoa wa Shinyanga maafisa kutoka migodi hiyo walisema katika kipindi cha mwaka 2011-2013 manunuzi kwa wafanyabiashara wazawa wanaozunguka mgodi yamekuwa hayana mtiririko endelevu,yaani yamekuwa yakishuka na kupanda lakini pia migodi yote imekumbwa na janga la kushuka thamani ya dhahabu sokoni ambapo kwa ujumla imepelekea migodi kupunguza matumizi ya mahitaji mbalimbali inayopelekea kupungua biashara kwa wafanyabiashara
Waandishi wa habari nao walikuwepo wa lutosha wakichukua mawili matatu kwa ajili ya kuufahamisha umma namna gani migodi inayopatikana katika mkoa wa Shinyanga inawanufaisha wananchi wake ambao asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo maisha yao yako duni sana ukilinganisha na utajiri wa mkoa
Huo ndiyo utaratibu wa manunuzi,ambapo sababu za msingi za kuwa na ununuzi wa ndani ni kushirikiana na wafanyabiashara wa ndani kuendeleza uchumi wa nchi,kutoa fursa katika ngazi ya jamii za kujishughulisha katika biashara ili kuongeza kipato katika familia,kuongeza fura za ajira,kuongeza ubora wa bidhaa zinazopatikana nchini,kuongeza ufanisi wa wagavi wa ndani na kuongeza pato la serikali kupitia kodi mbalimbali
Maafisa wa kutoka kampuni ya ABG walisema dhamira ya kampuni hiyo ni kufanya ununuzi wa ndani kwanza,kwa kuzingatia thamani bora kila iwezekanavyo ambapo  kanuni za ushindani bora zinajumuisha mambo mbalimbali kama vile gharama jumla ya bidhaa ama huduma,kuboresha huduma,mtazamo wa pamoja katika usalama,afya na mazingira na uendeshaji biashara katika misingi ya sheria ,taratibu na kiwango cha juu cha maadili
Wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo pia walipata nafasi ya kusimama na kuuliza maswali kwa maafisa wa migodi hiyo ya dhahabu iliypo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
Wafanyabiashara wanaofanya kazi na migodi hiyo hivi sasa pamoja wafanyabiashara wanaotegemea kuanza kufanya kazi na migodi hiyo wakisikiliza kilichokuwa kinajiri katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Karena mjini Shinyanga.
Mkutano unalekea ukiongoni

Picha za pamoja zikapigwa,hapa ni picha ya pamoja mkuu wa mkoa Ally Nassoro Rufunga na baadhi ya wafanyabiashara mkoani Shinyanga
Picha ya pamoja maafisa kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post