MWANAMKE MWENYE NDEVU KAMA MWANAMME ATISHIWA KUUAWA

Mwanamke huyo ambaye anakabiriwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki. 
Ameeleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina mengi ya kejeli kama ‘jike dume’, na kwamba alikuwa anashindwa hata kuwaangalia watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote asionekane mara kwa mara.
Ameongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua akafikiria kujiua.
Hata hivyo, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na kubatizwa, na kwamba imani ya dini hiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. 
Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na kifuani.
Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.
“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia. 
Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi.” Amesema Harnaam.
“nawezza kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi kuwa kule. Navaa skirts, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha zangu kama msichana mwingine yeyote.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post