MAPATO YA MBEYA CITY VS SIMBA HAYA HAPA

Mbeya City
Simba ya Jijini Dar es salaam 
Mapato kwa mechi ya ligi ya Vodacom kati ya timu za Mbeya City ya Jijini Mbeya na Simba ya Jijini Dar es salaam yamevunja rekodi ya michezo yote iliyowahi kuchezwa nje ya Jiji la Dar es salaam kwa kuingiza kiasi cha sh. milioni 105.
Mechi iliyowahi kuingiza kiasi kikubwa cha mapato katika uwanja huo ni ile iliyochezwa kati ya Timu ya Mbeya City na Yanga ya Dar es salaam katika uwanja huo mwaka jana na kuingiza kiasi cha sh. milioni 100.

Katika mapato hayo kila timu ilipata kitita cha sh. milioni 25.3 ambapo sh.milioni 12.8 zilibaki kwa ajili ya uwanja,sh.milioni 7.7 kwa ajili ya maandalizi na sh. milioni 7.7 kwa ajili ya kamati ya ligi ilhali sh. milioni 3.8 zilikuwa ni kwa ajili ya chama cha mpira wa miguu TFF.
Na Steve Kanyefu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post