January Makamba na Sugu washiriki kwenye wimbo wa hip hop wa kusisitiza sanaa kutambulika kwenye katiba mpya

Kilio cha wasanii kuitaka katiba mpya kuitambua sanaa ya Tanzania kama sekta rasmi kimepewa sapoti na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January makamba na mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bongo5, Makamba na Sugu wameshiriki kwenye wimbo wa hip hop uliowahusisha rappers 13 wa Tanzania, wimbo wenye lengo la kusisitiza sanaa kutambulika kwenye katiba mpya. Katika wimbo huo, January Makamba amefanya Intro na Outro imefanywa na Sugu.

Rappers walioshiriki kwenye wimbo huo uliopewa jina la ‘Haki’ ni Kala Jeremiah, Quck Rocker, G-Nako, Nikki wa Pili, Mwana Fa, Danny Msimamo, Profesa Jay, Gosby, Joh Makini, Fid Q na Kala Pina.
‘Haki’ imetayarishwa ndani ya Bongo Records na mtayarishaji mkongwe P-Funk Majani.

Kwa mujibu wa John Kitime, mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, wasanii wamepanga kuwa na mkutano na waandishi wa habari (press conference) na kuzindua wimbo huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments