Breaking News!! MADIWANI WAWILI WA CHADEMA WAJIUZULU NAFASI ZAO NA KUBAKI RAIA WA KAWAIDA SHINYANGA

Madiwani wawili wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo Cchadema)  katika  manispaa ya Shinyanga wametanganza rasmi kujiuzulu nyadhifa zo kutokana na madai ya uongozi ngazi ya taifa  kuendelea kusikiliza majungu,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwaita  wahaini au wasaliti katika chama  bila kuchambua ukweli na kutotekeleza waliyoyaahidi kwa wanachama wao.

Madiwani hao ni Sebastiani Peter (PICHANI) kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo ambao wamedai  wanayatamka rasmi maneno  mbalimbali yaliyopelekea kujiuzulu kama inshara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa kwa nyakati tofauti.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post