ZITTO KABWE ASHINDA HUKUMU YA KESI YAKE

Watanzania wengi hasa  wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA macho na masikio yao yalikuwa yameelekezwa  katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa   alikuwa  akitoa  hukumu  dhidi  ya  Zitto Kabwe  na CHADEMA....
 
Zitto ambaye alikuwa   ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho  iliyokutana  tarehe  3  na  4  mwezi  huu  kujadili  hatima  ya  uanachama wake  wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake... 

Akisoma  hukumu  ya  kesi  hiyo  baada  ya  kuiahirisha  jana, Jaji  wa mahakama  hiyo,Jaji Utamwa  ameridhia  pingamizi  lililotolewa  na  mh. Zitto Kabwe la  kutojadili  uanachama  wake na  kuitaka  kamati  kuu  ya  CHADEMA  au  chombo  kingine  chochote  kisijadili  uanachama  wake   hadi  kesi  yake  ya  msingi ( rufaa )  itakaposikilizwa  na  baraza  kuu  la  chama  hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post