Usiombe yakukute haya!!! SAMAKI AINGIA SEHEMU ZA SIRI ZA MSICHANA NA KUPOTELEA TUMBONI WAKATI AKICHOTA MAJI HUKO MKOANI MARA


Ukisikia maajabu ya dunia ama kali ya mwaka 2014 basi hii hapa,Samaki mwenye ukubwa wa nchi nne aingia tumboni mwa msichana kupitia sehemu za Siri za msichana huyo.

 Tukio limetokea huko Bunda mkoani Mara katika kijiji cha Bwanza siku ya jana.

Tukio hilo limetokea wakati msichana huyo akiwa amechuchumaa akichota maji kwa ajili ya kumwagilia bustani ya vitunguu lakini alishangaa kuona samaki akiruka kutoka ndani ya maji na kuingia sehemu zake za Siri na alipojaribu kumvuta alishindwa kutokana na maumivu ya kuchomwa na miba ya samaki huyo.

Samaki aliingia hadi kuzama kabisa hadi tumboni hali iliyopelekea msichana huyo kuanza kusikia maumivu makali ya tumbo mida ya saa 8 usiku na kisha kupelekwa hospitali na kudaiwa hana tatizo hivyo familia ya msichana huyo imempeleka mtoto wao kwa mganga wa kienyeji kwa tiba zaidi.

Habari kamili kuhusu tukio hili la aina yake inakuja……………..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post