NB Siyo mti aliojinyonga marehemu |
Mkazi mmoja wa kijiji
cha Maskati maarufu kwa jina la Maskati
Fisi kata ya Imesela katika wilaya ya
Shinyanga vijijini Njile Nkelembi(55-60 amekutwa
amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia chandarua katika mti wa
mwembe .
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja ambapo Njile
Nkelembi ambaye alikuwa anafanya kazi ya kuuza kahawa katika kijiji hicho alikutwa amejinyonga katika
shamba lake jirani na nyumba yake.
Akizungumza na malunde1.blogspot.com mwenyekiti wa kijiji hicho Hamis Salum amesema hadi sasa
hakuna sababu iliyopelekea kutokea kwa kifo hicho.
Naye Diwani wa kata ya Imesela Juma Kayumbo ameeleza kusikitishwa na taarifa ya kifo hicho
na kuongeza kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana waziwazi kwani
marehemu hakuacha ujumbe wowote na kwamba tayari mazishi yamefanyika.
Post a Comment